Ijumaa 24 Oktoba 2025 - 10:32
Maktaba ya Vatican yatenga sehemu kwa ajili ya Kufanya Ibada watafiti wa Kiislamu

Hawza/ Maktaba ya Vatican imetenga sehemu ndogo mahsusi kwa ajili ya watafiti Waislamu ili waweze kuswali wakati wanapoenda kufaya ziara zao za kitafiti.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, likinukuu IQNA, Padri Giacomo Cardinali, naibu wa Maktaba ya Vatican, katika mahojiano yake na gazeti La Repubblica, alieleza kuwa watafiti wa Kiislamu wenyewe ndio waliotoa ombi la kuwepo kwa sehemu hiyo.
Uongozi wa maktaba ulilikubali ombi hilo na ukaandaa ukumbi maalumu uliofunikwa kwa zulia ili kutumika kwa ajili ya jambo hilo.

Maktaba ya Vatican, iliyoasisiwa katikati ya karne ya kumi na tano, inahesabiwa kuwa moja ya vituo muhimu zaidi vya utafiti duniani.
Maktaba hiyo inahifadhi takribani nakala 80,000 za maandiko ya mkono (manuscripts), zaidi ya nyaraka 50,000 za kumbukumbu, karibu vitabu milioni mbili vilivyochapishwa, pamoja na mamia ya maelfu ya sarafu, medali, michoro na chapa.

Padri Cardinali alisisitiza kuwa maktaba hiyo pia inahifadhi nakala za zamani za Qur’ani Tukufu, sambamba na maandiko ya Kiebrania, Kihabeshi, Kiarabu na Kichina, jambo linaloonesha upana wa urithi wa kimataifa wa hazina hiyo.

Akaielezea maktaba hiyo kuwa ni “maktaba ya kimataifa”, iliyo wazi kwa watafiti wa mataifa yote na wa imani zote za kidini.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha